JE!UNAJUA MZUNGUKO WA MAISHA YA NYUKI?
Mzunguko wa maisha ya nyuki upo katika ngazi 4 yaani..(a)yai{egg} (b)kiluwiluwi{larva} (c)buu{pupa} (d)nyuki kamili{adult}.ukuaji huu unaanza na yai ambalo malikia anatunga na mara tu anapotoka kujamiiana na nyuki dume{drone}. Naukuwaji huu wa nyuki kutoka yai hadi kuwa nyuki kamili huwa una tofautiana na jinsia gani ya nyuki itakayo zalishwa.
kwani kuna aina 3 za makundi {caste} za nyuki 1.worker{kibarua} 2.malikia{queen} 3.nyuki dume{drone}.
zifuatazo ni hatua mabazo caste hawa hupitia kutoka yai hadi kuwa nyuki kamili.
1.worker{kibarua}
HATUA
(a)YAI{EGG}
-hapa yai linaanguliwa kwa muda (siku) 3.
(B)KILUWILUWI{LARVA}.
Katika hatua hii lava mabadiliko ya ngozi yana tokea mara 4 ila kwa muda (siku) tofauti.mageuzi ya kwanza ya ngozi muda (siku)3.5 , mara ya pili muda (siku) 4.5 ,mara ya tatu muda ( siku)6.5 ,mara ya nne ambayo ni badiliko la mwisho kwa hatua hii ya lava ambao huchukua muda (siku)6.5. baada yahapo chumba cha sega cha lava kinafunikwa na nta kwenye muda (siku)8-9.
(C)BUU{PUPA}
-Hapa mambo mawili hutendeka kwa muda(siku) tofauti.
*pupa hujizungushia mfuko wa nyuzi nyuzi muda (siku) 10.
*pupa kujigeuza ngozi kwa mara ya 5 muda (siku)11.
(D)NYUKI KAMILI{ADULT}
-Hapa mabadiliko ya ngozi yanafanyika kwa mara ya mwisho na kuwa nyuki kamili na mabadiliko hayo yanafanyika kwa muda (siku)20.
-Na wa muda(siku)21 anatoka nje ya chumba ambacho alikuwa analelewa na kuwa nyuki kamili.
2. MALIKIA{QUEEN}.
HATUA
(a) YAI{EGG}
- Muda (siku) 3 yai linaanguliwa.
(b) KILUWILUWI(LARVA)
-Hap mabadiliko ya ngozi yanatokea kwa muda (siku) tofauti kwani mbadiliko wa 1 hufanyika muda ( siku) 3.5 ,wa pili ni 3.5 , wa tatu ni 6.5 ,wa nne ni 6.5 , na baada ya hapo muda (siku) 8 chumba cha malikia{queen cell} kinafunikwa na nta .
(C)BUU{PUPA}
-Muda(siku) 10 anajizungushia mfuko wa nyuzi
-Na muda(siku) 10 anafanya tendo la kujigeuza ngozi kwa mara ya 5.
(D)NYUKI KAMILI{ADULT}.
-Muda (siku) 15 anajigeuza ngozi kutoka buu kuwa nyuki kamili -Muda (siku) 16 anatoka kwenye chumba chake {queen cell} teari kwa kujamiana na nyuki dume{drone}.
3.NYUKI DUME{DROME}.
HATUA.
(A) YAI{EGG}.
-Muda (siku) 3 yai linaanguliwa .
(B)KILUWILUWI{LARVA}
-Hapa lava anajigeuza ngozi mara 4 ila muda (siku) tofauti
*Kwa mara ya kwanza muda (siku)4
*Kwa mara ya pili muda(siku)5
*Kwa mara ya tatu muda(siku)7
*Kwa mara ya nne muda(siku)7
-Muda(siku)10 chumba cha nyuki dume kina funikwa na nta .
(C)BUU{PUPA}.
-Muda(siku)12 buu anajizungushia mfuko wa nyuzi nyuzi.
-Muda(siku)14 tendo lakujigeuza ngozi kwa mara ya 5 lina tendeka.
(D)NYUKI KAMILI{ADULT}.
-Hapa buu anajigeuza ngozi na kubadilika kuwa nyuki kamili muda(siku)225.
-Muda(siku) 24 nyuki dume (drone) anatoka nje ya chumba {drone cell} teari kujamiana na malikia{queen} .
No comments:
Post a Comment